Monday, 21 December 2015

EPUKA VITU HIVI 6 ILI KUONDOKANA NA TATIZO LA VIDONDA VYA TUMBOHabari za leo mdau wangu wa www.dkmandai.com naamini kwamba utakuwa vizuri huku tukiendelea kuzimalizia siku za mwezi Disemba mwaka huu 2015.

Vidonda vya tumbo ni matokeo ya uzalishaji wa tindi kali aina ya haidrokroliki asidi nyingi kupita kiasi ndani ya tumbo.

Tindikali hiyo huharibu utando wa ngozi nyembamba ndani ya tumbo kubwa na tumbo dogo.

Miongoni mwa vyanzo vya tatizo hili ni pamoja na hivi vifuatavyo:

1. Utumiaji wa vinywaji vya kusisimua  mwilini kama chai, kahawa, pombe  na madawa ya kulevya.
2. Kufanya kazi nyingi kupita kiasi tena bila kula.
3. Kutokuwa na ratiba maalum ya kula.
4. Kula vyakula vilivyokolezwa viungo.
5. Kuishi na msongo mkubwa wa mawazo 'stress
6. Uvutaji wa sigara kupita kiasi.

Ili kuepuka tatizo hili la vidonda vya tumbo ni vyema kuhakikisha unaepuka vile vyote ambavyo vipo kwenye orodha ya vichocheo vya tatizo la vidonda vya tumbo.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment