Tuesday, 1 December 2015

FAHAMU HUU UWEZO WA MAFUTA YA ALIZETI LEO


Mafuta ya alizeti ni miongoni mwa mafuta yatokanayo na mimea yanayotajwa kuwa na umuhimu wake kwa binadamu pia.

Leo napenda kuyazungumzia mafuta haya kwenye na faida zake kwenye matatizo ya ngozi kwani sehemu kubwa ya miili yetu ni ngozi kama tunavyofahamu.

Mafuta ya alizeti husaidia sana kupunguza chunusi kwani mafuta haya yana vitamin A, C, D na E zote ni muhimu kwa afya ya ngozi hivyo basi kwa mtu mwenye shida hiyo anaweza kutumia mafuta haya kwa kupaka sehemu yenye tatizo tu.

Aidha, mafuta ya alizeti pia huilinda ngozi dhidi ya mionzi hatari ya jua kutokana na kwamba mafuta haya huwa na vitamin E ya kutosha hivyo husaidia sana kumkinga mhusika dhidi ya mionzi hatari ya jua iitwayo 'ultraviolet' (UV) lakini pia ndani ya mbegu za alizeti kuna beta carotene ambayo hupambana na uharibifu wa ngozi na kumkinga mhusika dhidi ya saratani.

Maatumizi ya mafuta ya alizeti humsaidia pia mhusika kubaki na sura ambayo inalandana na umri wake, hii ni kwa sababu mafuta hayo yana vitamin E ya kutosha ambayo ni nzuri kwa ngozi.

Ahsante kwa kuendelea kuwa nasi kwa maelezo zaidi kuhusu mimea tiba au huduma zetu tupigie Mandai Herbalist Clinic kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com 

No comments:

Post a Comment