Monday, 21 December 2015

FAHAMU KITAKACHOTOKEA MWILINI MWAKO BAADA YA KULA TENDE 3 TU KILA SIKU


Watu wengi tunapokula vyakula mbalimbali au matunda huwa hatujali sana kuhusu umuhimu wake mwilini bali wengi huwa tunajali zaidi kuhusu ladha pekee.

Hivyo hivyo pia katika ulaji wa tende wengi wetu tende huwa tunakula tu lakini huwa hatujali nini faida zake au zinaumuhimu gani katika miili yetu, lakini hapa ninayo haya maelezo mafupi tu kuhusu tende. Karibu twende sote katika somo hili.

Wataalam wa masuala ya kitabibu wanasema kwamba ulaji wa tende tatu tu kila siku unatosha sana katika kujenga mwili wako kiafya.

Kwanza kabisa tende zina virutubisho vingi sana miongoni mwa hivyo ni pamoja na madini ya 'potassium', 'copper', nyuzinyuzi, 'vitamin B6', 'magnesium' na virutubisho vyote hivyo muhimu kwa pamoja unaweza kuvipata ndani ya mwili wako ikiwa utakula tende tatu tu kila siku.

Tende pia ni nzuri sana kwa kuboresha mfumo mzima wa umeng'enyaji chakula ndani ya mwili hii ni kutokana kuwa na nyuzinyuzi 'fiber' ambazo husaidia sana kumuondolea mhusika tatizo la ukosefu wa choo kabisa.

Pia tende zinaelezwa kuwa ni mojawapo ya kinga ya matatizo ya saratani ya utumbo, lakini pia tende hizi hizi zinauwezo mzuri wa kuwasaidia wale wenye shida ya tatizo la bawasiri (hemorrhoids)

Tende pia zinauwezo wa kupambana na matatizo ya kiharusi pamoja na shinikizo la juu la damu, hii ni kwa sababu ndani ya tende kuna madini ya magnesium ambayo moja ya faida zake mwilini ni kushusha kiwango kikubwa cha msukumo wa damu 'High Blood Pressure', lakini pia kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa na jarida la 'American Journal of Clinical Nutrition clearly' ilionesha kwamba tende ni nzuri sana katika kupunguza hatari ya kukumbwa na kiharusi.

Pamoja na hayo, tende huwasaidia kinamama wajawazito hii ni kutokana na utafiti uliowahi kufanyika kwa kinamama ambao walibakiza wiki 4 tu kabla ya kujifungua na kupewa tende kila siku matokeo yalionesha kuwa kinamama hao hawakupata shida kabisa wakati wa kujifungua lakini pia tende huwasaidia kinamama wajawazito kushindwa kupoteza uzito mara baada ya kujifungua,

Unaweza kumuuliza Tabibu Abdallaha Mandai maswali mengine zaidi kuhusu somo hili mpigie kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment