Thursday, 24 December 2015

FAHAMU KUHUSU TEZI DUME NA DALILI ZAKE ZA AWALI KABISA

Ikiwa tunaelekea mwishoni kabisa mwa mwaka 2015 na kuelekea mwaka 2016 naamini mwaka huu utakumbukwa sana kwa mambo mengi yaliyotokea, lakini pia mwaka huu 2015 ni mwaka ambao tunaweza kusema kwamba tatizo la saratani ya tezi dume ni moja ya matatizo ambayo pengine yalitajwa sana na kupatiwa ufafanuzi wa kina kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Lakini ukweli ni kwamba saratani ni moja ya magonjwa yasiyoambukiza na hutokea pale ambapo seli za tezi dume (prostate gland) husambaa sehemu nyingine za mwili.

Mbaya zaidi tatizo hili la saratani huweza kumpata mtu bila kuonesha dalili za moja kwa moja kwa muda mrefu sana hadi pale inapokuwa imeenea sana.

Pale dalili zinapoanza kuonekana basi matatizo mengine nayo hutokea ikiwa ni pamoja na uvimbe wa tezi dume.

Dalili za mwanzo za mwanzo ni pamoja na mhusika kukojoa mara kwa mara hasa wakati wa usiku, mkojo kutoka kidogo au kushindwa kutoka kabisa, kupata maumivu wakati wa kutoa manii, kukojoa mkojo wenye damu pamoja na kushindwa kuzuia mkojo, hasa unapocheka.

Pamoja na dalili hizo hapo juu mtu anaweza pia kuhisi maumivu makali ya kiuno, mbavu, na kwenye mapaja, kukosa hamu ya kula, kupungua uzito, hali ya kuchoka na wakati mwingine kutapika, miguu kuvimba na wakati mwingine miguu huweza kukosa nguvu.

Unaweza kuwasiliana nasi Mandai Herbalist Clinic kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkamandaitz@gmail.com ili kupata huduma zetu, kumbuka kuwa tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment