Thursday, 10 December 2015

FAHAMU MATATIZO YA MKOJO NA MAANA ZAKE ZA RANGI YA MKOJO


Kwa kawaida matatizo ya mkojo mchafu huweza kutofautiana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kutokana na sababu mbalimbali.

Mwili wako unahitaji kiasi fulani cha maji ili ufanye kazi vizuri, hivyo kutokunywa maji vya kutosha husababisha mkojo kuwa mzito na uliokolea sana. Mkojo ukiwa na rangi ya njano mpauko inaweza kumaanisha unakunywa maji sana au umemeza/kuchomwa vidonge/sindano.

Lakini baadhi ya dawa husababisha kubadili rangi ya mkojo na kuufanya uwe kijani au bluu iliyofifia, ulaji wa karoti hufanya mkojo kuwa na rangi ya machungwa, wakati vitamini mbalimbali hufanya mkojo kuwa njano.

Mkojo ukibadilika na kuwa mwekundu hii ni ishara kuwa kuna damu kwenye mkojo lakini ni vyema ukafahamu kuwa ukiwa na damu chache mwilini mwako kunaweza sababisha mabadiliko makubwa ya rangi ya mkojo wako.

Aidha mkojo kuwa na harufu kali hii inaweza kumaanisha una ugonjwa au mawe kwenye njia ya mkojo (urinary stones),pia wagonjwa wa kisukari, wanaweza kuona mkojo wao una harufu tamu kutokana na sukari ya ziada kwenye mkojo wao.


Kwa kawaida watu wengi hukojoa mara 6 hadi 8 kila siku, lakini unaweza kukojoa mara nyingi zaidi kulingana na kiasi gani cha maji umekunywa.

Ikiwa unahisi kukojoa mara kwa mara na hukunywa ugiligili wa kutosha kukojoa mara kwa mara, hii inaweza kuwa inasababishwa na maambukizi ya njia ya mkojo (UTI), ugonjwa wa kibofu, ugonjwa unaosababisha kibofu kuvimba na kufanya mtu ahisi kibofu kimejaa na kutaka kukojoa mara kwa mara, magonjwa ya kuvimba tezi dume, kisukari, magonjwa ya mfumo wa fahamu kama Kiharusi (Stroke)

Ikiwa mtu haendi kukojoa vya kutosha hali hiyo huweza kutokana na mirija kuziba au maambukizi au inaweza kuwa ni kwa sababu ya tabia iliyojengeka ya kujizuia kwenda haja mara kwa mara. Kuchelewa kukojoa au kubana mkojo kunaweza kusababisha matatizo kwenye kibofu kwa sababu ya kulazimishwa kibofu kusinyaa hata kama mkojo umejaa.

Ili kulinda kibofu chako kunywa maji kwa ukawaida na sio kunywa sana maji. Kunywa maji, kila unapohisi kiu na sio kujilazimisha kunywa maji labda kama umeshauriwa na daktari au una ugonjwa wa mawe kwenye kibofu.

Wasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment