Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Thursday, 31 December 2015

FAHAMU NAMNA UNAVYOWEZA KUTUMIA KIUNGO CHA ILIKI KUJITIBU


Habari za Alhamis hii ya Desemba 31, 2015 ikiwa ni siku ya mwisho kabisa ndani ya mwaka huu, sina shaka utakuwa unaendelea vizuri mdau wangu wa www.dkmandai.com.

Kwa sasa naomba nitumie nafasi hii kukufahamisha haya machache kuhusu faida za matumizi ya iliki.

Hapa duniani Mwenyezi Mungu ametujalia vitu mbalimbali ambavyo vikitumika vizuri huweza kuwa na thamani sana katika maisha yetu ya kila siku hususani katika kujenga afya zetu.

Iliki ni moja ya kiungo ambacho wengi wetu tunakifahamu sana na huenda huwa tunakitumia karibu kila siku kwenye shughuli za mapishi ya jikoni hususani katika kuandaa chai, lakini licha ya kwamba ni kiungo tu pia kina faida zake kwa afya.

Moja ya faida za matumizi ya iliki ni pamoja na kusaidia kuipa uwezo mzuri figo wa kuondoa taka mwili ndani ya mwili, huku ikisaidia sana kuweka sawa mfumo wa umeng'enyaji wa chakula tumboni.

Iliki pia husaidia sana kuondoa kiungulia, gesi tumboni pamoja na kuwasaidia wale wenye shida ya kukosa choo ‘constipation’ kwa muda mrefu.

Aidha, iliki imekuwa ikisifika sana kwa uwezo wake wa kusaidia kuweka sawa harufu ya kinywa, pamoja na kutibu shida ya vidonda vya mdomoni pamoja na matatizo yote ya kinywa na koo.


Iliki ambayo imetolewa ganda lake la nje
Pia iliki inauwezo mzuri sana wa kutibu matatizo ya maambukizi kwenye njia ya mkojo sambamba na kupambana na magonjwa mbalimbali.

Iliki pia inauwezo wa kukabilina na hali ya mambukizi ya mafua sambamba na kikohozi, huku ikisifika kwa kuondoa maumivu ya viungo mwilini.

Mbali na hayo, iliki pia inauwezo mzuri wa kukabiliana na matatizo ya saratani, pamoja na presha.

Kama unapenda zaidi kujua mimea tiba na matumizi ya lishe bora basi jitahidi ufika Mandai Herbalist Clinic tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam au wasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment