Tuesday, 15 December 2015

FAHAMU SABABU ZA KUWASHWA SEHEMU ZA SIRI KWA WANAUME NA WANAWAKE NA JINSI YA KUPAMBANA NAYO

Tatizo la kuwashwa sehemu za siri ni moja ya tatizo ambalo linawasumbua watu wengi sana yaani wanaume na wanawake pia.

Lakini kuna mambo ambayo huweza kuchangia mhusika kupatwa na muwasho sehemu za siri mara kwa mara.

Hata hivyo, ili kuepuka tatizo hili tukianza na wanaume jambo la msingi mwanaume kuhakikisha kuwa anaosha vizuri uume na kwa wale ambao hawajafanyiwa tohara wanapaswa kuosha kwa umakini zaidi hadi sehemu za ndani (govi.)

Mbali na hayo sehemu za siri zinapaswa kuwaa katika hali ya usafi na ukavu muda wote, hii ni kwasababu unyevunyevu unaweza sababisha maambukizi.

Pia hakikisha unavaa nguo isiyobana sana na nzuri iwe imetengenezwa kwa pamba, lakini pia ni vyema ukajenga utaratibu wa kubadili nguo ya ndani angalau kila siku. 

Kwa upande wa wanawake  wao wanapaswa kufunya haya ili kuepuka matatizo ya kuwashwa sehemu za siri

Kwanza ni kuhakikisha baada ya kujisaidia unanawa sehemu zako za siri kuanzia mbele (ukeni) kwenda nyuma  ili kuzuia bakteria kutoka njia ya haja kubwani kuingia ukeni.

Epuka matumizi ya vitu vyenye kemikali sehemu za siri kama marashi katika kusafisha, kwa kufanya hivyo tambua utakuwa unaharibu hali ya asili ya sehemu za siri (uke) na kuua bakteria wanaolinda uke na kufanya iwe vyepesi kushambuliwa na maradhi.

Hakikisha unajikausha vizuri maji maa baada ya kujisafisha sehemu zako za siri na epuka kukaa na nguo mbichi kwa muda mrefu.

Vaa nguo isiyobana sana, iliyotengenezwa kwa pamba ili unyevunyevu usitokee na hakikisha unajitahidi kubadili nguo mara kwa mara.

Ukiona bado unaendelea kuwashwa tu hata baada ya kufuata njia hizo hapo juu ni vyema ukaonana na wataalam wa afya kwa ajili ya matibabu zaidi na ushauri wa matibabu.

Mbali na hayo ni vyema ukakumbuka kuwa siku zote  usafi humfanya mwanamke na mwanaume kujiamini wakati wote.

Pia unaweza kupata ushauri wa kitabibu kutoka kwa mtaalam wa tiba asili kutoka Mandai Herbalist Clinic Tabibu Abdallaha Mandai mpigie kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com


No comments:

Post a Comment