Tuesday, 22 December 2015

HII NDIO JUISI PEKEE AMBAYO HUWEZA KUMSAIDIA MWANAMKE MWENYE MATATIZO YA HEDHI

Kwa kawaida kipindi cha hedhi huwa ni kati ya siku nne hadi saba, huku siku mbili za kwanza damu hutoka kwa wingi na baadaye huanza kupungua na hatimaye kuacha.

Lakini iwapo katika siku zote za hedhi damu ikatoka kwa wingi na ikaendelea kutoka kwa siku zaidi bila kuashiria dalili za kuacha basi lazima kuwe na tatizo linalohitaji kupatiwa ufumbuzi.

Hata hivyo, kuna baadhi ya wanawake kuna wakati hujikuta wakipata hedhi mapema zaidi tofauti na matarajio yao au mtiririko wao wa kawaida, hii hali nayo huwa ni tatizo na huhitaji kupatiwa ufumbuzi au kuonana na wataalam kwa ushauri zaidi.

Pamoja na hayo, ikiwa umekumbwa na tatizo la kutokwa na damu za hedhi kwa muda mrefu unaweza kutumia komamanga kama huduma ya kwanza kwako.

Unachopaswa kufanya ni kutengeneza juisi ya tunda la komamanga , kisha kunywa glasi moja asubuhi wakati wa kifungua kinywa.
Anza tiba hii siku tatu kabla ya muda wa hedhi, ikiwa tayari unalijua tatizo lako na endapo lilishatokea siku za nyuma.

Endelea na tiba hiyo hadi siku mbili mbele mara baada ya damu kuacha kutoka.

Endapo unasumbuliwa na tatizo hili ni vyema ukawasiliana sasa na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment