Wednesday, 23 December 2015

HII NDIO NCHI AMBAYO IMEPITISHA MATUMIZI YA BANGI KWA MATIBABU


Rais wa Colombia , Juan Manuel Santos, ametia sahihi sheria mpya inayohalalisha matumizi ya bangi kwa manufaa ya kimatibabu

Kupitia hotuba yake kwa njia ya runing bwana Santos alisema kuwa sheria hii kimsingi inaiweka Colombia katika mstari wa mbele wa kupamabana na matumizi ulanguzi na ukuzaji wa bangi Kusini mwa Marekani.

"Tumechukua hatua ya kwanza kuisadia Colombia kupambana na gonjwa hili sugu la matumizi ya mihadarati."

Pamoja na maamuzi yake hayo bwana Santos alisisitiza kuwa sheria hiyo mpya haikinzani hata kidogo na mswada wake wa kupambana na mihadarati, huku akisema kuwa 
kufaidi uwezo wa utabibu wa bangi kwa hakika haizuii kwa vyovyote msimamo wetu dhabiti wa kupambana na matumizi ya mihadarati.''

"Sheria hiyo mpya inaruhusu ukuzaji wa mmea huo kwa wale tu waliopewa idhini na serikali''

No comments:

Post a Comment