Tuesday, 8 December 2015

HUU NDIO UWEZO WA BOGA KATIKA KUREKEBISHA NGOZI YA MWILI WAKOBoga ni mojawapo ya tunda zuri na lenye virutubisho vingi ambavyo vyote ni muhimu sana kwa afya ya miili yetu.

Kama utakuwa ni mfuatiliaji wa masomo yangu mara kwa mara kupitia tovuti hii nadhani utakuwa unakumbuka kuwa mara kadhaa tumeshazungumza sana kuhusu faida za boga kwa ujumla, lakini hiyo haizuii kuendelea kuzungumzia sifa za boga leo tena.

Leo napenda tuzungumzie uwezo wa boga katika kuboresha afya ya ngozi zetu kamaifuatavyo>>

Kwanza kabisa unapotumia boga husaidia sana kuleta unyevunyevu kwenye ngozi na hivyo kuwasaidia wale wenye matatizo ya ngozi kavu hii ni kutokana na kuwa na vitamin E ya kutosha pamoja na kirutubisho kiitwacho 'antioxidant '

Maboga pia yana vitamin A yakutosha ambayo husaidia sana kuilinda ngozi dhidi ya kuharibiaka na kuunda seli mpya pia ndani ya ngozi.

Lakini pia ndani ya boga kuna vitamin C ambayo nayo huhitajika sana katika kuhakikisha afya ya ngozi inakaa vizuri zaidi siku zote 

Hayo ni machache kuhusu afya ya ngozi na matumizi ya boga, lakini kwa mengine mengi unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment