Thursday, 17 December 2015

JE, MATATIZO YA KUNUKA MIGUU YANAKUKWAZA? FAHAMU NAMNA YA KUKABILIANA NA TATIZO HILO HAPAMiguu kutoa harufu mbaya ni tatizo ambalo linawakabili baadhi ya watu katika jamii hususani wanaume.

Kuna mambo ambayo unaweza kuyafanya na yakawa msaada kwako kwa wewe mwenye tatizo hili, njia hizo ni kama ifuatavyo.

Kwanza ukigundua unatatizo hilo, hakikisha unasafisha miguu yako mara kwa mara na kuikausha vizuri kabisa ili kuepusha unyevunyevu.

Pili kila unapovaa viatu vya kufunika hakikisha unavaa soksi safi na zilizo kauka vizuri.

Epuka kurudia soksi kabla ya kufua au ambazo hazijakauka vizuri kwani huweza kuchangia miguu kunuka zaidi.

Usivae viatu vilivyoloa na endapo ikatokea umenyeshewa, hakikisha unavianika kwenye hewa ili vikauke ili kupunguza uwezekano wa kutoa harufu.

Hata hivyo licha ya kuwepo kwa sababu mbalimbali zinazochangia tatizo hili la kunuka miguu, ukweli utabaki kuwa uchafu ndio chanzo kikuu cha miguu kutoa harufu.

Endapo utahisi tatizo ni kubwa zaidi basi unaweza kuwaona wataalam ili kupata ushauri na tiba zaidi.

Karibu Mandai Herbal Clinic, tupo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam au wasiliana nasi kwa mawasiliano yafuatayo 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment