Saturday, 19 December 2015

JE, UNAJUA MADHARA YA KUKOSA MUDA WA KULALA?


Je, unafikiri ni muda gani ni sahihi wa kulala kwa siku? ni masaa mangapi unadhani ukiyatumia kwa kulala utakuwa umeutendea haki mwili wako.

Wataalam wa afya wanashauri kuwa binadamu anapaswa angalau kupata mapumziko ya kulala angalau masaa 7 hadi 8 wakati wa usiku ili kuupa mwili afya bora.

Kwa kawaida kulala kwa masaa machache au kutolala huweza kusababisha matatizo ya kiafya ikiwa ni pamoja na shinikizo la damu  pamoja na mwili kubaki mchovu.

Kufuatia hali hiyo ni vyema ukahakikisaha unatumia muda wako vizuri mchana ili usiku upate muda mzuri wa kutosha kwa kulala na kupumzika ili kuepukana na matatizo ya kiafya japo kuwa najua kwamba mazingira yetu ya kimaisha yanatulazimisha kupunguza muda wetu wa kulala hivyo tunapopata nafasi ni vizuri kuitumia kwa kupumzika.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment