Tuesday, 1 December 2015

JE, UNAYAFAHAMU HAYA KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO?


Ugonjwa wa vidonda vya tumbo hutokea iwapo kidonda cha ukubwa wa angalau wa nusu sentimita kitatokea kwenye sehemu yeyote ya ukuta wa tumbo au utumbo wa binadamu. Kwa kawaida tatizo hili huleta maumivu makali sana ya tumbo ingawa si lazima kila maumivu ya tumbo yakawa ni vidonda vya tumbo.

Tatizo hili huchangiwa na maambukizi ya bakteria aina ya Helicobacter Pylori. Aina hii ya vimelea vya bacteria husababisha karibu asilimia 60 ya vidonda vinavyotokea kwenye tumbo (gastric ulcers) na zaidi ya asilimia 90 ya duodenal ulcers.

Maambukizi hayo huharibu mfumo na uwezo wa kuta za tumbo kutunza homoni ya Gastrin, ambayo ni muhimu katika kuhakikisha mazingira ya tumbo yanakuwa na kiwango salama cha tindikali.

Aidha tatizo hili huweza pia kuchangiwa na matumizi ya muda mrefu ya dawa za kuondoa maumivu za kundi la NSAIDs: Ukuta wa utumbo hujilinda na madhara yatokanayo na tindikali ya utumbo. Dawa hizi za kundi la NSAIDs huharibu mfumo wa kutengeza vichocheo hivi yaani prostaglandins na hivyo kufanya kuta za tumbo kukosa utando wa kuzilinda na mashambulizi ya tindikali hali ambayo hupelekea kutokea kwa vidonda vya tumbo.

Uvutaji wa sigara nayo ni moja ya sababu ya tatizo hili. Uvutaji sigara sambamba na maambukizi ya bakteria aina ya Helicobacter pylori huongeza madhara ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo lakini ni vyema ikafahamika kwamba uvutaji sigara pekee hausababishi vidonda vya tumbo.

Unywaji wa pombe: Unywaji wa pombe pekee hausababishi vidonda vya tumbo. Hata hivyo, unywaji wa pombe sambamba na maambukizi ya vimelea vya Helicobacter pylori huongeza madhara ya tatizo hili zaidi.

Hayo ni machache kuhusu tatizo hili lakini kama unasumbuliwa na vidonda vya tumbo kwa muda mrefu unaweza kufanya jitihada ya kupata dozi ya Likolo (pichani hapo juu) ambayo itamaliza kabisa tatizo hilo au piga simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment