Thursday, 17 December 2015

JE, UNAZIJUA FAIDA ZA UNGA WA NGANO KATIKA TIBA ? ZIPO HAPA

Unga wa ngano wengi wetu tunaufahamu sana na tumekuwa tukiutumia katika mapishi ya vitafunwa mbalimbali tuwapo nyumbani.

Lakini si wengi yunafahamu kama unga wa ngano unaweza kusimama kama tiba ya tatizo lolote, lakini ukwelii ni kwamba unga wa ngano huweza kuwa tiba ya tatizo la kuwashwa mwilini.

Tunapozungumzia matatizo ya kuwashwa mwili basi huweza kuwa sehemu yoyote ya mwili na inaweza kuwa ni matokeo ya tatizo fulani lililoko mwilini, kama vile mzio (allergy) minyoo.

Mwili unapowasha kunaweza kuwa ni dalili za ugonjwa unaohitaji kuchunguzwa na kutibiwa  badala ya kutafuta kutibu dalili za ugonjwa.

Hata hivyo, kumekuwa na tiba asilia mbalimbali za tatizo hilo ambazo ni pamoja na soya, ndimu, komamanga , unga wa ngano pamoja na majani ya ngano, lakini katika tiba zote hizo leo hii tutaelezea hii tiba ya kutumia  unga wa ngano ambayo pengine inaweza kuwa ni rahisi kwa wengi.

Unachopaswa kufanya katika kutumia unga wa ngano kama tiba ni kupaka unga wa ngano sehemu zote za mwili zinazowasha na hakikisha unatumia tiba hii kwa muda wa siku 10.

Iwapo bado tatizo linaendelea baada ya kutumia tiba hiyo basi jaribu tiba ya aina nyingine. Au fika Mandai Herbalist Clinic, Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam pia unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallaha  Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com. 

No comments:

Post a Comment