Tuesday, 22 December 2015

JINSI MCHANGANYIKO WA MAZIWA NA ASALI UTAKAVYOKUSAIDIA KUONDOSHA MIKUNJO MWILINI MWAKOKatika maisha yetu binadamu tunavyoishi kila siku zinavyozidi kwenda basi kwa kawaida mabadiliko hujitokeza ndani ya miili yetu moja ya mambo hayo ni pamoja na mabadiliko ya ngozi pia.

Miongoni mwa mabadiliko hayo ni pamoja na ngozi kuana kutengeneza mikunjo hasa mikononi na shingoni pia.

Leo hapa ninayo mbinu itakayokusaidia kuondosha mikunjo mwilini mwako karibu twende sote hapa.

Matumizi ya maziwa na asai yanatosha kabisa kuondosha tatizo hilo ikiwa utafanya haya yafuatayo:

Kwanza kabisa kwa kawaida maziwa na asali vyote kwa pamoja ni bidhaa muhimu kwa afya ya ngozi zetu.

Maziwa huwa na masaada mkubwa wa kuondosha madoa mwilini, lakini asali yenyewe msaada wake ni katika kuhakikisha inaifanya ngozi inabaki kuwa na unyevunyevu wakati wote.

Namna ya kuandaa asali na maziwa ili ya kusaidie kuondosha mikunjo inabidi upate nusu kikombe cha maziwa pamoja na vijiko viwili vikubwa vya asali na kijiko kimoja cha sukari.

Baada ya kuvipata vyote hivyo utachanganya kwa pamoja kisha tumia kwa kupata sehemu zenye mikunjo mwilini mwako kisha acha mchanganyiko huo mwilini mwako kwa dakika 20 kisha nawa kwa maji ya vuguvugu.

Fanya zoezi hilo kwa muda wa wiki mbili kila siku kutwa mara mbil, lakini kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com
2 comments:

  1. VP ukitumia kama kinywaji mchanganyiko huo Wa asali na maziwa

    ReplyDelete
  2. VP ukitumia kama kinywaji mchanganyiko huo Wa asali na maziwa

    ReplyDelete