Thursday, 3 December 2015

KESI ILIYOKUWA IKIMKABILI ALIYEKUWA MWENYEKITI WA CUF PROF IBRAHIM LIPUMBA NA WAFUASI 30 IMEFUTWA RASMI

LIPUMBA ii
Professor Ibrahim Lipumba alikuwa na kesi pamoja na wafuasi 30 wa CUF katika Mahakama ya Kisutu Dar es Salaam akikabiliwa na mashtaka ya kufanya mkusanyiko bila ya kuwa na kibali cha Polisi.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa toka January 2015, lakini kwa mujibu wa ripoti kutoka kwenye taarifa ya habari ya ITV inasema  kwamba Prof. Lipumba na watu wote 30 wamefutiwa mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili Mahakamani hapo.

No comments:

Post a Comment