Wednesday, 2 December 2015

KITUNGUU MAJI HUTIBU TATIZO LA KUPATA HAJA NDOGO YENYE KUAMBATANA NA MAUMIVU


Kitunguu maji ni moja ya kiungo ambacho hutumiwa sana na binadam karibu kila siku, hasa katika shughuli za jikoni, lakini kiungo hiki pia ni tiba kwa matatizo ya afya zetu.


Mtaalam wa tiba asili Dk Abdallah Mandai anaeleza kwamba kwa wale wenye shida ya haja ndogo (mkojo) kuuma anaweza kuponda kiasi cha gramu sita ya vitunguu na baadaye kuchemsha katika nusu lita ya maji na kuiacha ichemke hadi pale itakapo pungua nusu ya ule ujazo wote kisha apatiwe mgonjwa anywe.

Pia mtaalam huyo anabainisha kwamba matone ya maji ya kitunguu huweza kusaidia kuwa dawa ya sikio na kusaidia kuondoa milio yote ya sikioni na tatizo hilo litaacha.

Matatizo mengine yanayoweza kutatuliwa na kiungo hiki ni pamoja na kikohozi, vidonda vya tumbo, ngozi, figo pamoja na tumbo.


Dk Mandai anasema kuwa, kwa tatizo la kikohozi kinachotakiwa kufanyika ni kuchukuwa kitunguu maji kimoja kikubwa na ukikate kate kwenye maji kisha chemsha maji hayo dakiaka tano na baadaye mgonjwa anywe kijiko kikubwa kimoja kutwa mara tatu yaani asubuhi mchana na jioni.


Kwa maelezo zaidi wasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment