Tuesday, 15 December 2015

MAMBO YA KUEPUKA KWENYE MAKUZI YA VIJANA NA MAHUSIANO


Kipindi cha ukuaji wa vijana huwa na changamoto nyingi kwani mwili unakuwa tayari kwa ngono na viungo vya uzazi vinakuwa tayari kwa uzazi.

Kundi la vijana wanaobalehe linajumuisha wasichana na wavulana wenye umri wa kati ya miaka 10 hadi 19.

Hii hutokea baada ya homoni ya 'testosterone' (Testosterone) na istrodioli (Oestrodiol) kuanza kuzalishwa mwilini.

Vijana wa kike na wa kiume wanapokuwa husababisha mabadiliko mengi kwa vijana ikiwa ni pamoja na wasichana kukua matiti, kuota nywele sehemu za siri kwa jinsia zote mbili, kukua kimaumbile, kupatwa na chunusi. Vijana hujihisi wamekuwa na kujitambua zaidi kitu kinachosababisha kuanza tabia mpya hatarishi kama kuvuta sigara, kunywa vileo mbalimbali na kujihusisha na vitendo vya ngono.

Wasichana wengi huanza balehe kati ya miaka 8 hadi 14, hivyo umri wa wastani wa balehe kwa wasichana ni miaka 11. Kimsingi, wasichana hukua haraka zaidi kuliko wavulana ambapo wavulana hubalehe kati ya miaka 9 na 14, umri wa wastani wa balehe kwa wavulana ukiwa ni miaka 12. Balehe imekuwa ikiwahi kwa miaka ya hivi karibuni tofauti na miongo michache iliyopita.

Mabadiliko wanayopata vijana wakati wa balehe hasa ya kimaumbile na kihisia huwafanya wawe wepesi kutaka kujaribu vitu vipya ambavyo hawakuwahi kuvifanya hapo mwanzo mfano kuvuta sigara, kunywa pombe na kufanya ngono. Kutamani kufanya ngono huchochewa na picha na video zenye habari za ngono wanazoona ambazo wakati mwingine husababisha ndoto nyevu kwa vijana.

Ni vyema vijana wakatambua madhara ya kuanza ngono mapema zaidi ili waweze kukabili tamaa zao za ngono mpaka wakati utakaowafaa kuweza kufanya ngono.

Yapo madhara mbalimbali ambayo kijana huweza kuyapata kwa kuanza ngono mapema na kwa namna moja au nyingine huweza kukwamisha mipango mbalimbali ambayo amekuwa akijiwekea katika kukamilisha malengo yake. Na maradhi hayo ni kama yafuatayo:

Mimba za Utotoni

Miili ya wasichana inaweza ikawa imekua kuweza kushika mimba ila maungo yao ya uzazi kama nyonga yanaweza yasiwe yamekomaa kuweza kujifungua salama hivyo huweza kusababisha kifo kwa mabinti.

Pia wajawazito watoto wana hatari zaidi ya kupatwa na kifafa cha mimba na mtoto kukwama kwa kuwa msichana anakuwa hajakua vya kutosha maungo yake ya uzazi hasa nyonga.

Magonjwa ya ngono/ Zinaa
Mara nyingi siku ya kwanza kufanya ngono, watoto waliobalehe wanakuwa hawana elimu kuhusu ngono na uzazi. Vilevile wengi huwa wanajaribu ili kujua jinsi inavyokuwa, hivyo kuwa hawajajiandaa kutumia kondomu au njia zingine za uzazi wa mpango. Wasichana waliobalehe wanakuwa hawana nguvu, ujasiri na mbinu bora za kukataa vishawishi vya kufanya ngono hivyo upelekea kufanya ngono isiyo salama inayoweza kuwasababishia maradhi ya zinaa.

Angalizo:
Ni vyema watoto waliobalehe wakaepuka ngono za mapema ikiwa ni pamoja na kuwa na kuepuka makundi ambayo si mema.

Kwa ushauri zaidi na mawasiliano unaweza kumpigia Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment