Thursday, 17 December 2015

MATATIZO YA FANGASI SEHEMU ZA SIRI

Fangasi sehemu za siri (ukeni) husababishwa na fangasi aina ya 'Candida Albanians'. Ugonjwa huu huitwa 'vaginal candidiasis' kwa kiingereza na ni kati ya magonjwa ambayo husumbua wanawake mara kwa mara.

Fangasi ya ukeni huambukizwa kwa njia ya kutumia vyoo vichafu pamoja na kuchangia nguo za ndani na taulo.
Joto pia unyevu mwingi na nguo za kubana huchangia pia kutokea kwa fangasi ukeni. Ugonjwa huu unaweza kuambukizwa kwa njia ya ngono.

Dalili za ugonjwa huu ni pamoja na kutokwa na maji maji meupe mfano wa maziwa kutoka kwenye uke ambayo hayana harufu mbaya, kuwashwa sehemu za siri hasa kwenye uke na mashavu ya uke.

Dalili nyinginezo ni maumivu wakati wa kupata haja ndogo (kukojoa) kwa baadhi ya wagonjwa. Mara chache hali hii hutokea, ikisababishwa nakuchubuka wakati wa kujiwasha na kujikuna.

Hata hivyo, ili kuepukana na tatizo hili ni vyema kuzingatia usafi wa nguo za ndani kwa kuvaa nguo safi iliyofuliwa kila siku na kuanikwa juani (au kupigwa pasi).

Pia vaa nguo za ndani zilizokauka vizuri. Epuka zenye unyevunyevu au mbichi.

Hali kadhalika ni vizuri ukazingatia usafi wa sehemu za siri na kujikausha vizuri mara baada ya kuoga. Huku pia usafi wa choo ukizingatiwa na kuimarishwa.

Kama unasumbuliwa na tatizo hili kwa muda mrefu sasa ni vizuri kufika kituo cha afya na  ukawaona wataalam wa afya, lakini pia unaweza kufika Mandai Herbalist Clinic ukaonana na Tabibu Abdallaha Mandai au mpigie kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment