Thursday, 3 December 2015

POKEA HIZI FAIDA ZA KUTUMIA CHENZA MARA KWA MARA


Chenza ni moja ya tunda lenye ladha nzuri sana na lenye kupendwa na watu wengi wakiwemo watoto na watu wazima pia.

Tunda hili wengi wetu tumekuwa tukilitumia sana huenda kutokana na kupenda ladha yake tu, lakini hili ni moja ya tunda ambalo pia lina faida nyingi katika miili yetu.

Miongoni mwa faida za chenza ni pamoja na kusaidia kuongeza vitamin C mwilini kama ilivyo katika chungwa, pia husaidia kuongeza nguvu kwenye misuli na kuimarisha mifupa.

Tunda hili pia husaidia kuzuia uvujaji wa damu katika fizi, na huondoa maumivu ya viungo sambamba na kuwasaidia wale wenye udhaifu wa kuona.

Mbali na hayo, pia chenza huwasidia wale wenye tatizo la mawe ya figo na kibofu, viuvimbe chini ya tumbo na inatibu unene wa mirija ya damu.

Matumizi yake katika tiba ni wewe kuzingatia kula kila unapoweza kulipata tunda lake.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

1 comment: