Tuesday, 1 December 2015

RAIS MAGUFULI AAMUA PESA ZA SIKU YA UHURU ZITUMIKE KUPANUA BARABARA YA MWENGE HADI MOROCCORAIS John Magufuli ameamuru fedha zilizopaswa kutumika kugharimia shamrashamra za Sikukuu ya Uhuru Desemba 9, mwaka huu, kutumika kupanua barabara ya Mwenge hadi Morocco jijini Dar es Salaam, yenye urefu wa kilometa 4.3 kwa kuongeza njia mbili za barabara za lami.

Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa kwa vyombo vya habari jana, ilisema tayari fedha hizo, kiasi cha Sh bilioni nne, zimepelekwa kwa Wakala wa Barabara (TANROADS) kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo, linalopaswa kuanza mara moja.

Akizungumza na Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Patrick Mfugale, Ikulu, Dar es Salaam jana, Rais Magufuli alitaka ujenzi wa barabara hiyo uanze haraka ili kukabiliana na adha ya msongamano wa magari katika barabara hiyo.

Kujengwa kwa njia hizo, kutaifanya barabara ya Morocco hadi Mwenge kuwa na njia tano. Rais Magufuli hivi karibuni alitangaza kufuta maadhimisho ya Sikukuu ya Uhuru, ambayo huadhimishwa kwa kufanyika kwa gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama kwenye Uwanja wa Uhuru.

Badala yake, mwaka huu maadhimisho hayo yafanyike kwa watu kufanya kazi za usafi katika maeneo yao ya kazi na majumbani. Akiwa katika kampeni za uchaguzi mkuu, Rais Magufuli aliahidi kumaliza tatizo la foleni za barabaran

No comments:

Post a Comment