Thursday, 24 December 2015

SABABU 10 ZITAKAZO KUWEKA KATIKA HATARI YA KUKUMBWA NA SHINIKIZO KUBWA LA DAMU (PRESSURE)Shinikizo kubwa la damu ni ongezeko la nguvu ya msukumo wa damu katika mishipa inayochukua damu kutoka kwenye moyo kwenda kwenye viungo na tishu mwilini.

Kiwango cha kawaida cha shinikizo la damu mwilini ni 120/80mmHg au chini yake. Pale kiwango kinapokuwa 140/90mmHg au zaidi hali hiyo huwa ni shinikizo kubwa la damu.

Kimsingi tatizo hili huwa halina dalili za wazi na ndio maana matatizo haya huitwa 'silent killer' 

Pamoja na kwamba tatizo hili huwa halioneshi dalili za moja kwa moja lakini kuna mambo kadhaa ambayo huweza kuongeza uwezekano wa mhusika kupata shinikizo kubwa la damu na hapa ninayo 'list' ya mambo hayo:

1. Kuwa na umri wa zaidi ya miaka 40
2. Kuwa na uzito uliozidi kiasi
3. Kuwa na msongo wa mawazo (stress)
4. Kuwa na historia ya shinikizo la kubwa la damu katika familia yako
5. Kuwepo na matatizo mengine ya kiafya mwilini, kama magonjwa ya figo, matatizo ya mishipa ya damu, magonjwa ya moyo, kisukari au saratani
6. Kuwa na jinsia ya kiume, kwasababu huwapata wanaume zaidi kuliko wanawake
7. Matumizi ya chumvi kwa wingi au vyakula vyenye chumvi nyingi
8. Matumzi ya baadhi ya dawa hasa bila ushauri wa wataalam
9. Utumiaji wa pombe na uvutaji sigara
10. Ujauzito

Huenda utakuwa na swali au maoni basi usisite unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment