Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Monday, 28 December 2015

SABABU ZA TATIZO LA UZAZI KWA KINABABA NA JINSI YA KUKABILIANA NALO KWA KUTUMIA VYAKULA

Matatizo ya ugumba kwenye familia nyingi huelekezwa zaidi kwa kinamama na imekuwa ni nadra sana matatizo haya kuelekezwa kwa kinababa japo kuwa wao pia huweza kuwa na shida hii ya ugumba.

Nimekuwa nikipokea maswali mbalimbali kutoka kwa wanaume wakiomba angalau kujua sababu kadhaa ambazo huchangia tatizo la ugumba kwa wanaume.

Miongoni mwa sababu ambazo huchangia tatizo la ugumba kwa wanaume ni pamoja na kukaa sehemu sehemu yenye joto kali sana kwa muda mrefu au kufanya kazi kwenye mazingira yenye kemikali zinazoathiri uzalishaji wa mbegu za kiume.

Sababu nyingine ni tabia ya unywaji pombe kupindukia na uvutaji wa sigara sambamba na matumizi ya madawa ya kulevya kama kokeni, bangi jambo ambalo hupunguza idadi na kiwango (quality) cha shahawa . 

Tatizo hili pia huweza kuchangiwa na kukosekana kwa baadhi ya vichocheo mwilini madhara yatokanayo na magonjwa ya korodani au kwenye mishipa ya korodani.

Magonjwa mengine ambayo huweza kuchangia mwanaume kuwa na tatizo la uzazi ni pamoja na kuzongwa na magonjwa ya ngono kwa muda mrefu pamoja msongo wa mawazo.

Sasa ili kuepuka tatizo hili inashauri kupendelea kutumia vyakula asili katika mlo wako kila siku na kuacha kutumia vyakula vya makopo hii ni kwa sababu vyakula asili mara zote huwa na virutubisho asili ambavyo huusaidia mwili kujijenga vizuri na kumfanya mhusika kuwa vizuri hata katika afya ya uzazi.

Jenga utaratibu sasa wa kula mboga za majani, matunda na vyakula vyenye asili ya mzizi nazungumzia mihogo, magimbi pamoja na viazi, lakini pia epuka matumizi ya vyakula vilivyopikwa kwa kutumia mafuta mengi.

Kwa maelezo zaidi au ushauri wa tatizo hili unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com


No comments:

Post a Comment