Friday, 4 December 2015

TAARIFA KUHUSU AJALI YA GARI LA MAGAZETI YA MWANANCHI (RIP)Kupitia mitandao ya kijamii hususani kwenye facebook, whatsapp na instagram imeenea taarifa taarifa inaonekana gari ya magazeti ya mwananchi imepata ajali na kunatajwa kuwa kuna watu wamefariki pia kwenye ajali hiyo.

Nimempata Mhariri wa gazeti la Mwananchi, Frank Sanga ambaye amesema yuko mkoani Tanga kikazi lakini taarifa alizozipata ni kwamba gari lililopata ajali ni gari ambalo lilikodiwa na Kampuni hiyo ya Magazeti kupeleka Magazeti Mbeya… mazingira ya ajali inaonesha gari hilo liligonga lori kwa nyuma, na madereva wote wawili waliokuwa ndani ya gari wamefariki.

Ajali hiyo imetokea maeneo ya mlima Kitonga mkoa wa Iringa.

#RIP kwa marehemu wa ajali hiyo.

Chanzo: Millard ayo.com

No comments:

Post a Comment