Friday, 11 December 2015

TAARIFA KUTOKA IKULU KUHUSU RATIBA YA KUAPISHWA KWA MAWAZIRI NA MANAIBU MAWAZIRI


Jana Disemba 10/205 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk John Pombe Magufuli alitangaza rasmi baraza lake la mawaziri, licha ya kwamba kuna wizara alisema bado hajazipatia mawaziri wake ikiwa ni pamoja na iliyokuwa wizara yake hapo awali wizara ya ujenzi.

Taarifa iliyonifikia kutoka ofisi ya kurugenzi ya mawasiliano ya Rais, Ikulu kuwa Mawaziri na Manaibu Waziri walioteuliwa jana Dec 10, 2015 na Rais wa awamo ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli wanatarajiwa kuapishwa siku ya Jumamosi Dec 12, 2015 ikulu Dar es Salaam.

Shughuli hizo za uapishwaji zitafanyika kuanzia saa tano asubuhi.

Chanzo: Millard ayo.com

No comments:

Post a Comment