Thursday, 3 December 2015

TABIBU MANDAI: JENGA AFYA YA FAMILIA YAKO KWA KUZINGATIA MPANGILIO HUU WA VYAKULA


Moja ya sababu inayoweza kuchangia magonjwa yasiyo ya lazima katika afya zetu ni pamoja na kutozingatia ulaji mzuri wa vyakula .Hivyo ni vizuri tukafahamishana baadhi ya mambo muhimu ya kuzingatia katika kupangilia vyakula.

Tabibu Abdallah Mandai, anasema kwamba, miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na kuhakikisha unatenganisha mboga na matunda, hii inamaana kuwa ni vizuri ukajenga tabia ya kula matunda kwa wingi katika saa yake, huku ukijitahidi kula mboga pia kwa wakati wake, hii ni kwa sababu si vizuri kuchanganya vitu hivi kwa pamoja, mfano mzuri ni pale mtu anapokula mboga zikiwa pamoja na ndizi, mtu huyu huwa na nafasi kubwa ya kuweza kupatwa na kiungulia.

Pia mtaalam huyo anaendelea kueleza kuwa, ni vizuri kuwa na ratiba ya kula na kuzingatia suala la kubadilisha chakula chako kutoka mlo hadi mlo kwa kufuata ratiba utakayokuwa umeipanga, jambo la msingi ni kuhakikisha hauli aina nyingi ya vyakula katika mlo mmoja.

Aidha, Tabibu Mandai alisema unapotenga muda maalum wa kupata mlo kila siku, hii husaidia myeyusho wa chakula kwenda vizuri zaidi tofauti na yule ambaye anakula pasipo kuwa na ratiba maalum.

Kwa kusisitiza hili la mlo Tabibu Mandai hapa anatumia mfano huu kufafanua ambapo anasema “asubuhi kula kama mfalme, mchana kula kama malkia na jioni kula kama masikini, hii inamaanisha kwamba kifungua kinywa (breakfast) chako kinatakiwa kuwa kizuri na cha kutosha na mchana unatakiwa uwe ni mlo wa kawaida, lakini jioni ni vizuri ukapata mlo ambao ni mdogo na mwepesi na mlo huo ni vyema ukaliwa kuanzia saa 2 au 3 kabla ya kuelekea kulala.”

Aidha, ni vizuri ukazingatia kutumia vyakula vyenye nyuzi nyuzi pamoja na nafaka zisizokobolewa , hii ni kwa sababu vyakula vya aina hiyo ni bora zaidi kwa afya.

Vyakula ambavyo hukobolewa sana huwa havifai sana kwa afya na hata pale mchele unapooshwa sana huweza kusababisha kuondoka kwa baadhi ya virutubisho muhimu.
Jambo jingine ambalo ni zuri kwa afya yako ni kuzingatia kula kile unachokipenda ili kustawisha afya na furaha yako, lakini zingatia kutokula kupita kiasi, kwani unapokula sana huweza kujikuta ukiwa mchomvu na kuzongwa na usingizi pamoja na kupunguza hata uwezo wa kufikiri.

Pia epuka matumizi ya vikolezo vyenye madhara, ambavyo ni pamoja na sukari, chumvi na mafuta ni vizuri ukahakikisha vitu hivyo unatumia kwa kiwango kidogo sana.

Hata hivyo, inaelezwa kwamba viungo vya kukoleza chakula na madawa ya kuumulia vitu vyenye asili ya ngano vitu hivyo si vyakula bora kwani vingi husababisha madhara mbalimbali ya kiafya katika mwili wa mlaji.

Hali kadhalika maji pia ni muhimu katika kukamilisha suala la mlo, hivyo ni vizuri ukanywa maji ya kutosha yaliyo safi na salama na inapendekezwa angalau glasi 8 hadi 10 kwa kutwa nzima , lakini zingatia usinywe maji wakati wa mlo au muda mfupi sana kabla ya kula. Muda sahihi wa kunywa maji ni dakika 30 kabla na baada ya kula hii husaidia myeyusho wa chakula kufanyika vizuri.

Zingatia.
Tabibu Mandai anaeleza kuwa, wakati mwingine ni muhimu kujenga mazoea ya kutokula mlo mmoja au miwili ili kuruhusu viungo kupata muda wa kupumzika na kutengeneza dawa ya kuutibu mwili unaoelemewa na mizigo ya chakula kila siku. Hivyo kufunga ni msaada katika kudhibiti tamaa ya chakula pia kufunga ni dawa bora kwa magonjwa mengi hususani kwa watu wasiofanya kazi za mikono.

Karibu sasa Mandai Herbalist Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam kwa kufanyiwa uchunguzi wa afya yako na utakutana na huduma bora na  nzuri kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment