Wednesday, 2 December 2015

TABIBU MANDAI LEO ANAKUPA UFAFANUZI KUHUSU FAIDA ZA MTI WA MBUYU


Habari yako mdau wangu wa www.dkmandai.com asante sana kwa kuendelea kuwa karibu na toviti hiii kila siku na ukiendelea kupata masomo mbalimbali kuhusu tiba kila siku.

Leo tunaendelea kukumbushana mengine kuhusu mimea tiba na matunda mbalimbali na hapa leo napenda kuzileta kwako faida za mbuyu.

Mbuyu ni kati ya miti mikubwa na minene inayopatikana katika ukanda wa tropiki, Matunda yake yanaitwa mabuyu, gamba la tunda hilo huitwa kibuyu na ubuyu ni nyama ya tunda.

Mti wa mbuyu kimsingi umesheheni malighafi nyingi na nzuri katika afya ya binadamu, ambapo inaelezwa kuwa unga wa ubuyu huwa na vitamin nyingi na madini mengi, kwani unga huo una kiasi cha vitamin C nyingi kushinda ile inayopatikana kwenye tunda chungwa.

Tabibu Mkuu kutoka Mandai Herbalist Clinic Tabibu Abdallah Mandai anabainisha kuwa mti huo wa mmbuyu husaidia kutibu homa, ambapo mgonjwa atapaswa kuchemsha magome ya mmea huo na kunywa.

Pia Tabibu Mandai anaeleza kuwa mti huo unauwezo wa kutibu ugonjwa wa malaria, kifua kikuu pamoja na pumu pale magome yake yanapotumika mara baada ya kuchemshwa na mhusika kunywa.


Pamoja na hayo, Tabibu Mandai anafafanua kuwa kwa wale wenye shida ya kikohozi wanapaswa kuchanganya unga wa tunda lake pamoja na asali kisha mgonjwa atalamba au kutumia kwa kuchanganja na maji ya moto.


Hayo ni machache tu, lakini kwa undani zaidi ni vyema ukawasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai mwenyewe kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300,0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment