Friday, 4 December 2015

UWEZO WA KABEJI KWENYE TATIZO LA VIDONDA VYA TUMBO

Ugonjwa wa vidonda vya tumbo si tatizo geni miongoni mwa watu wengi kwani wengi wetu tunalifahamu tatizo hili huenda kutokana na kuwa nalo sisi wenyewe au ndugu zetu wa karibu, marafiki na wapenzi wetu kwa ujumla.

Ugonjwa huu hutokea mara baada ya mhusika kupata vidonda kwenye kuta za utumbo wa mwanadamu ambavyo hutokana na kuzidi kwa tindikali yenye kazi ya kuyeyusha chakula mwilini.

Kuna mambo kadhaa ambayo huweza kupelekea tatizo hili ikiwa ni pamoja na msongo wa mawazo, aina ya vyakula, kutozingatia muda wa kula na mfumo wa maisha yetu ya kila siku kwa ujumla.

Hata hivyo, wataalam wa afya wanaeleza kwamba chanzo cha tatizo hili ni kutokana na bakteria anayejulikana kama 'Helicobacteria pylori'.

Ni wazi kwamba kuna mambo mengi sana ya kuzungumza kuhusu hili tatizo la vidonda vya tumbo, kwani naamini kuna baadhi ya watu wangependa kufahamu dalili zake na hata kujua mambo ya kufanya ili kujiondoa katika hatari ya kukumbwa na tatizo hili naomba nikuahidi kwamba endelea kufuatilia tovuti hii ya www.dkmandai.com na nitakuletea hayo yote siku zijazo, lakini kwa siku ya leo mimi naomba nikwambie kuwa kabeji inauwezo wa kuwa msaada wako kwa vidonda vya tumbo ikiwa utafanya haya yafuatayo:

Tafuta kabeji na uikatekate kisha isage kwenye mashine ya kutengenezea juisi, baada ya hapo chuja na kisha kunywa kikombe kimoja cha chai cha juisi hiyo mara mbili kwa siku.

Kama utakuwa hujaelewa vizuri na utahitaji ufafanuzi zaidi wasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment