Wednesday, 30 December 2015

VIFAHAMU VIASHIRIA HIVI VINAVYOONESHA KUWA MWANAMKE YUPO TAYARI KUSHIKA UJAUZITO


Habari za leo mdau wangu wa www.dkmandai.com naamini utakuwa upo vizuri siku hii ya leo.

Naomba kuchukua muda wako mchache kwa ajili ya kufahamishana haya mambo muhimu ambayo huashiria mwanamke kuwa yupo tayari kwa asilimia nyingi kushika ujauzito.

Somo hili litawasaidia wale ambao wamekuwa wakitamani kuwa na watoto lakini hawafahamu ni siku gani sahihi ya kufanya tendo hilo la ndoa na wenzi wao ili kuweza kufanikisha kubeba ujauzito.

Sasa leo ninavyo viashiria ambavyo humaanisha mwanamke yupo katika hatari ya kuweza kushika ujauzito yaani 'ovulation period'

Kwanza kabisa mwanamke anapokuwa tayari kushika ujauzito huanza kuhisi hamu ya kushiriki tendo la ndoa, wanawake wanapokuwa katika siku zenye uwezekano mkubwa wa kushika mimba  matamanio yao ya kufanya mapenzi huwa ni makubwa zaidi kuliko ilivyo kawaida. Sasa huo ndio wakati unaofaa ikiwa unahitaji kubeba mimba au unahitaji mke wako abebe mimba.
Kupanda kwa joto la mwili, hii ni moja ya alama maarufu ambayo hutumiwa na wanawake wengi Ongezeko hilo la joto husababishwa na homoni ya 'progesterone', ambayo huongezeka sana
mara baada ya 'Ovulation'

Kubadilika kwa majimaji ya ukeni, wakati mwanamke anapokuwa katika uwezekano wa kushika mimba maji ya ukeni nayo huongezeka na kubadilika na kuwa katika hali ya majimaji na wakati mwingine huwa na rangi nyeupe kama yai bichi. Awali maji hayo ya ukeni huwa na rangi kama ya cream na hutoka kidogo sana na wengine hushindwa kuyaona kabisa.

Maumivu kwenye matiti, baadhi ya wanawake wakati wanapokaribia kwenye 'ovulation' huweza kuhisi maumivu kwenye matiti. Hata hivyo njia hii sio yenye kutegemewa sana kwani maumivu ya matiti huweza kusababishwa na masuala mengine kwani maumivu ya matiti hutokea kabla ya hedhi au baada ya kutumia baadhi ya dawa za kusaidia uzazi.
Ikumbukwe kwamba dalili zote hapo juu si lazima zitokee zote kila mwanamke huweza kuona dalili kati ya moja.Kuuelewa vyema mwili wako ni jambo zuri linaloweza kukusaidia kuzijua siku zako za 'Ovulation' na hivyo kuweza kujua siku zako za kubeba mimba.

Kwa ushauri na maelezo zaidi wasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment