Friday, 18 December 2015

VITU VINAVYOCHOCHEA TATIZO LA UPUNGUFU WA HAMU YA TENDO LA NDOA


Kuna baadhi ya wanawake wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo la ukosefu wa hamu ya kushiriki tendo la ndoa lakini leo hapa Mandai Herbalist Clinic chini ya usimamizi wa Tabibu Abdallaha Mandai ameona akufahamishe baadhi ya vitu vinavyochangia tatizo hilo.

Matumizi ya Pombe 
Licha ya kwamba baadhi ya watu wanapokunywa pombe huonekana wakizidi kupata matamanio zaidi ya tendo, lakini kwa asilimia kubwa watumiaji wa pombe husababisha kukosa hamu ya tendo la ndoa kabisa.

Matumizi ya Kahawa 
Kwa kawaida kahawa humfanya mtu kuwa mchangamfu na kumuongezea nguvu kwa muda mfupi lakini kutumia kahawa mara nyingi au mara kwa mara huweza kusababisha madhara kwenye kiungo kinachoitwa ARDENAL GRAND na kusababisha ubongo na mwili wako ujazwe kichocheo kiitwacho CORTISOL ambacho huleta uchovu mwingi katika mwili wako jambo ambalo linaweza kusababisha upotevu wa hamu ya tendo.

Matumizi ya Vyakula vya Kukaanga
Vyakula vya kukaangwa katika mafuta mengi hasa vinapotumika mara kwa mara huweza kuleta uchovu mwilini na huweza kupunguza ubora wa mbegu za kiume na afya ya yai kwa wanawake katika viungo vya uzazi wa mwanamke.

Uchovu
Kufanya kazi bila ya kupumzika au mawazo magumu husababisha kichocheo cha CORTISOL kumiminwa katika mfumo wa damu na kupunguza nguvu ya vichocheo vingine vinavyohusika na tendo la ndoa na sio hilo tu bali pia uchovu huweza kusababisha pia upungufu wa nguvu za kiume. Pamoja na hayo ukosefu wa usingizi nao huleta matokeo hayo hayo kwani nalo hilo hutibua kichocheo cha CORTISOL.

Kwa ushauri na maoni zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment