Wednesday, 16 December 2015

WALIOSAFIRI NJE BILA KIBALI CHA RAIS WASIMAMISHWA KAZI, TAKUKURU NAKO HAKUKALIKI RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU, (VIDEO)


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dk John Pombe Magufuli ameamua kutengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Dk Edward Hoseah baada ya kuona hakuna kilichofanyika katika miaka yote ya tangu makontena yalipoanza kupotea bandarini.

Aidha Mheshimiwa Rais Dk John Magufuli pia amewasimamisha kazi watumishi wanne ambao walikaidi agizo la rais na kuamua kusafiri bila kupata kibali cha rais au cha Katibu Mkuu Kiongozi.

Watumishi hao ni Ekwabi Mujungu, Doreen Kapwani, Rukia Nikitas na Mary Mosha ambao wote walisafiri nje ya nchi licha ya kutokuwa na kibali cha safari kutoka kwa rais, hivyo Rais ameagiza wafanyakazi hao kusimamishwa kazi

Ninayo video ya Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue hapa akielezea kuhus maagizo hayo ya Rais Dk John Magufuli  hapa chini>>>

No comments:

Post a Comment