Saturday, 19 December 2015

WATU 12 WAPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI YA BASI LA NEW FORCE (PICHA)


IMG_20151218_154336
Watu kumi na mbili wamefariki dunia na wengine kumi na nane wamejeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiri mali ya kampuni ya New Force kupata ajali baada ya kugongana na lori maeneo ya Kilolo mkoani Iringa.
IMG-20151218-WA0132

Jeshi la Polisi limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa chanzo chake ni baada ya lori kupoteza mweleko na kuligonga basi hilo.


Basi hilo la Kampuni ya New Force lilikuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Tunduma, na lori la mbao lilitoka Njombe kuelekea Dar es Salaam. 

IMG_20151218_154446

IMG-20151218-WA0130

Mwenyezi Mungu awapumzishe kwa amani waliofariki kwenye ajali hiyo na kuwapatia ahueni mapema majeruhi wote. R.I.P


No comments:

Post a Comment