Wednesday, 16 December 2015

WAZIRI WA MAGUFULI ATOA SAA 48 KWA WAUZA MADAWA YA KULEVYA


Kasi ya serikali ya awamu ya tano chini ya rais Dk John Pombe Magufuli imeonekana kuwa na kasi zaidi baada ya mawaziri wake wapya nao kuonekana kuanza kasi ya hapa kazi tu.


Leo Disemba 16, 2015 Waziri wa mambo ya ndani Charles Kitwanga amefanya ziara ya ghafla leo katika makambi mbalimbali ya Jeshi la Polisi na kutoa amri kwa viongozi wa jeshi hilo siku mbili za kuhakikisha amepata taarifa kuhusu udhibiti wa dawa za kulevya.

“Wapo wajanja wana mbinu nyingi, lakini hawawezi kutuua. Na mimi hili ni jambo nitalivalia njuga, lakini kwanini katika ukamataji wa dawa za kulevya sisi tulioko kwenye operesheni tunakaa pembeni? Nataka jibu siku ya Ijumaa”


Mbali na hayo, Waziri ameonekana kuguswa na tabia ya kubambikiziwa kesi, ambapo waziri amesema “Hili la kubambika watu kesi tunaweza kuliondoa hata leo, kikubwa ni kuwa na nidhamu, inakuwaje unambambika mtu kesi ili akuletee pesa? Hiki ni kitendo cha rushwa na tuliangalie kwa pamoja na tutaliongea kwa undani Ijumaa”

No comments:

Post a Comment