Thursday, 10 December 2015

YAFAHAMU MAMBO MUHIMU YATAKAYOFANYA SEHEMU ZAKO ZA KIUME KUWA IMARA NA AFYASiku zote ili mwanaume aitwe mwanaume aliyekamilika ni lazima sehemu zake za siri yaani uume  ziwepo (Penis).

Sehemu za siri za mwanaume (uume) ni kiungo muhimu sana kwa jinsia ya kiume na ni kiungo chenye hisia.

Kwa kawaida wanaume wengi wamekuwa wakitumia kiungo hicho pasipo kuzingatia usafi na utunzaji wake na hivyo kufanya sehemu hizo nyeti kuwa chafu na baadaye kutoa harufu mbaya.

Sasa leo kama ilivyo kawaida yetu kupitia tovuti hii ya www.dkmandai.com naomba tufahamishane umuhimu wa kutunza uume.

Jenga tabia ya kusafisha uume wako mara baada ya kutoka haja, lakini pia hakikisha unaosha mikono yako wakati wowote kabla ya kugusa uume wako. Hii ni kutokana kushika vitu vingi ambapo kunakuwa na uwezekano mkubwa wa kutunza kemikali. 

Jichunguze mara kwa mara
Kuwa na utaratibu wa kuangalia sehemu zako za siri kama kuna uvimbe wowote na pia kwa ishara ya magonjwa ya zinaa. Kuchunguza pia shahawa zako ili kutambua mabadiliko yoyote katika muonekano au uwepo wa damu katika uume.

Hakikisha uume wako haupatwi na majeraha
Muda wote epuka sehemu yako ya siri kupatwa na majeraha ya mara kwa mara kwani huweza kuathiri ubora wa uume wako pamoja na utendaji kazi wake pia.
.
Kuwa na mwanamke mmoja
Kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja huweza kuleta madhara kwa afya ya uume wako, lakini pia kuwa na mwanamke mmoja kutakusaidia kuwa na nguvu na uwezo mzuri wakati wa kufanya tendo la ndoa na hasa kabisa kujikinga na magonjwa ya zinaa.

Kunywa maji  yakutosha
Jenga tabia ya kunywa angalau glasi nane za maji safi. Maji husaidia sana kufanya mzunguko wa damu kuwa mzuri ndani ya mwili hivyo kusaidia kuongeza msisimko mwilini.

Kwa ushauri zaidi wasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment