Tuesday, 8 December 2015

YAFAHAMU MAMBO MUHIMU YATAKAYOKUSAIDIA KUPATA MTOTO KIRAHISI KWENYE NDOA YAKO

Familia ili ikamilike na iwe na amani siku zote inahitaji kuwa na mtoto au watoto tatizo huweza kutokea pale ambapo wanandoa watahitaji kuwa na watoto halafu ikawa ni swala gumu kutokana na sababu mbalimbali.

Hata hivyo kwa kawaida huwa kuna sababu mbalimbali zinazoweza kuchangia wanafamilia kushindwa kupata mtoto, lakini hapa ninazo njia kadhaa ambazo zitakusaidia angalau kujiweka katika nafasi nzuri ya familia yako kupata mtoto.

Mambo ya kuyazingatia ni haya yafuatayo>>>>

Zingatia kudumisha uzito unaofaa kiafya
Kwa sasa wanawake wengi hujikuta wakishindwa kudhibiti uzito wa miili yao na kujikuta wanakuwa na uzito uliokithiri jambo ambalo huweza kuleta uzito kwenye masuala afya ya uzazi. Hii ni kwa sababu uzito unaweza kuathiri udhibiti wa homoni na hivyo kuathiri uzalishaji wa mayai.

Ubora wa mbegu za kiume.
Ili mwanaume abaki kuwa na uwezo mzuri wa kutungisha ujauzito ni lazima apate vyakula vyenye virutubisho vyenye uwezo wa kurutubisha mbegu za kiume, lakini pia ili kuwa na mbegu zenye afya, wanaume wanahamasishwa kudumisha uzito unaofaa kiafya, kula mlo bora na kamili, kuzuia magonjwa ya ngono, kudhibiti msongo wa mawazo (stress) na kufanya mazoezi.

Epuka uvutaji wa sigara
Ili kujiwekakatika mazingira ya kuweza kushika mimba na kuweza kusababisha mimba ni lazima kuepuka kutumia sigara na kudhibiti matumizi ya pombe jambo ambalo huweza kuleta uzito kwenye masuala ya uzazi.

Ni vyema kuvaa nguo za ndani zisizobana sana, tumia muda kidogo kukaa, kuepuka joto sehemu za siri mfano kukaa kwenye jakuzi la maji moto, kuweka simu au kompyuta za kupakata (laptops) karibu na korodani.

Epuka kabisa magonjwa ya ngono
Magonjwa ambukizi (ya ngono) ni hatari sana kwenye masuala ya uzazi na miongoni mwa magonjwa hayo ni pamoja na kisonono, kaswende ambayo kwa kiasi kikubwa huharibu mfumo wa uzazi kwa kinababa na kinamama.

Jitahidi kukutana na mwenzi wako kindoa
Ikiwa unapendana upo tayari ndani ya ndoa yako kuanza kupata mtoto basi ni vyema mkajenga utaratibu wa kukutana kindoa mara nyingi iwezekanavyo hasa wakati wa siku nzuri kwa mwanamke kushika ujauzito. Kwa wastani, siku nzuri za mwanamke kupata mimba kwenye mzunguko wa hedhi huhusisha siku 5 kabla ya ovulesheni(yai kutolewa), siku ya ovulesheni na siku 2-3 kufuatia ovulesheni.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment