Wednesday, 23 December 2015

ZABIBU HUSAIDIA KUONDOA TATIZO LA KUKOSA CHOO NA HATARI YA KUPATWA NA PUMU

Habari za leo mdau wangu wa www.dkmandai.com sina shaka utakuwa ni mzima kabisa na unaendelea vizuri na shughuli zako za kila siku kama utakuwa na matatizo ya kiafya kidogo basi naomba nikupe pole pia.

Leo napenda tuzungumze kuhusu zabibu ni mojawapo ya matunda matamu yanayopendwa pia, huku yakiwa na faida nyingi kiafya na hapa nchini Tanzania matunda haya hupatikana zaidi Dododoma.

Zabibu ambazo wengi wentu tumezoea kuziona na ambazo tunazifahamu pia ni zile zabibu za rangi nyeusi, lakini ni vyema ikafahamika kuwa pia kuna zabibu za rangi ya kijani na nyekundu pia.

Matunda ya zabibu ndiyo matunda pekee ambayo hutumika kutengenezea mvinyo 'wine' sehemu mbalimbali duniani.

Miongoni mwa faida za zabibu kiafya ni pamoja na kusaidia kuweka sawa mmeng'enyo wa chakula na hivyo kumsaidia mhusika kuondokana na tatizo la kukosa choo.

Zabibu husaidia kuongeza unyevunyevu kwenye njia ya hewa na hivyo kupunguza uwezekano wa utokeaji wa pumu.

Ndani ya zabibu kuna madini chuma ambayo ni madini muhimu kwa kujenga mifupa imara na kusaidia sana kuongeza damu mwilini kutokana na kuwa na madini chuma.

Zabibu pia husaidia sana kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo pamoja na saratani na kusaidia kuzuia mafuta kulundikana kwenye mishipa ya damu.

Huenda utahitaji maelezo zaidi kuhusu somo hili basi unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment