Wednesday, 23 December 2015

ZAMBARAU INAWEZA KUBORESHA TENDO LA NDOA KWA WANAUME NA WANAWAKE

Tabibu Abdallaha Mandai ni mtaalam wa tiba za mimea na mitishamba kupitia kituo chake kiitwacho Mandai Herbalist Clinic inayopatikana Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

Leo napenda kukutanisha na Tabibu Abdallaha Mandai ambapo anakuelezea namna mti wa mazambarau unavyoweza kutumika kama tiba. Karibu tuwe sote.

Kuhusu mizizi ya mzambarau Tabibu Mandai anasema ukiichimba na kuchemsha kisha ukatumia kwa kunywa glasi moja asubuhi na jioni kila siku hiyo huweza kuwa njia nzuri ya kuwasaidia kinamama wenye shida ya kutoona siku zao, licha ya kwamba hawajafikia muda wa kufunga hedhi yaani 'menopause'

Magome ya mzambarau Tabibu Mandai anasema husaidia sana kuimarisha kinga za mwili na kuwasaidia kinababa wenye shida ya nguvu za kiume, kinachofanyika ni kupata magome na kuyakausha kisha kuyasaga halafu utatumia unga huo wa magome kwa kupima kijiko cha mezani ndani ya maji ya uvuguvugu au uji kila siku asubuhi na jioni na itakusaidia sana.

Pia unga huo wa magome nao huweza kuwasaidia wenye tatizo la kisukari kwani husaidia sana kusawazisha kiwango cha sukari mwilini, lakini si kutibu kisukari bali kuweka sawa kiwango cha sukari mwilini.

Hata hivyo Tabibu Mandai alieleza pia kuhusu ugonjwa wa bawasiri au mgolo (kuota kinyama sehemu ya haja kubwa) ambao nao unaweza kutibika kwa kutumia majani ya mzambarau kinachofanyika ni kuchemsha majani ya mzambarau na utayaacha yapoe kisha utatumia maji hayo kwa kunawa sehemu ya haja kubwa.

Lakini kwa maelezo zaidi unaweza kumtafuta Tabibu Abdallaha Mandai ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mandai Herbalist Clinic kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800

No comments:

Post a Comment