Wednesday, 9 December 2015

ZIFAHAMU HIZI FAIDA ZA PARACHICHI MWILINI MWAKO

Bila shaka parachichi ni miongoni mwa matunda yenye ladha tamu na ni maarufu duniani kote. Kutokana na utamu na wingi wake wa mafuta, unaweza kudhani siyo tunda zuri kiafya, lakini ukweli ni kwamba ni miongoni mwa matunda mazuri sana kiafya.

Tunda hili limesheheni virutubisho takriban 20 ambavyo ni muhimu sana kwa ustawi wa afya zetu. Tafiti zimeonesha kuwa watu wenye tabia ya kula tunda hili kwa wingi huwa na afya njema na uzito unaokubalika.

Ingawa parachichi lina mafuta mengi, lakini ni mafuta mazuri (Monousaturated) ambayo yana uwezo wa kupunguza hatari ya mtu kupatwa na kiharusi au ugonjwa wa moyo.

Mbali ya kuwa ni tunda lenye mafuta mengi, lakini tafiti zinaonesha linaweza kusaidia katika zoezi la mtu kupunguza uzito, kwani kwa kula kipande kimoja tu na chakula kiasi mchana, mtu hujisikia ameshiba kwa muda mrefu, hivyo kumuondolea hamu ya kutaka kula mara kwa mara.

Baadhi ya kazi za parachichi ni pamoja na:
Kupunguza uzito (Weight Loss), kudhibiti shinikizo la damu (Blood Pressure), Kushusha kiwango cha lehemu (Lower Cholesterol Levels), kudhibiti ugonjwa wa kisukari (Diabetes), kuondoa maumivu ya viungo (Pain Relief), magonjwa ya kuvimba (Inflamations) na huimarisha nguvu ya jicho kuona (Eye health).

Faida zingine ni pamoja na kuimarisha mifupa ya mwili, husaidia usagaji wa chakula tumboni, pia lina kiwango kingi cha kirutubisho aina ya Folate Acid, parachichi linafaa kuliwa kwa wingi na ni zuri sana kuliwa kwa kina mama wajawazito.

Ndani yake kuna  virutubisho vya aina mbalimbali karibu 20. Baadhi ya virutubisho hivyo ni pamoja na Vitamin C (33%), Vitamin B6 (26%), Vitamin E (21%), Pantothenic Acid (28%), Copper (19%), Potassium (28%), Vitamin K (53%) na Folate.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment