Wednesday, 30 December 2015

ZIFAHAMU SABABU ZA WANAWAKE KUPATA MAUMIVU MAKALI WAKATI WA TENDO LA NDOA


Kuna baadhi ya wanawake wamekuwa wakipata maumivu makali wakati wanaposhiriki tendo la ndoa jambo ambalo huchangia wanawake wenye tatizo hilo kushindwa kufurahia kabisa tendo hilo.

Maumivu hayo hutokana na hali ya mabadiliko ukeni ambapo uke huwa mkavu daima au mwanamke anapata vipindi vya ukavu ukeni na katika mlango wa kizazi.

Maumivu hayo huweza kuwa ndani ya kizazi au chini ya kitovu na kiuno wakati wa tendo lakini pia maumivu hayo yanaweza kutokea baada ya tendo la ndoa. Mwanamke anaweza kushiriki tendo la ndoa vizuri lakini mara anapomaliza tu akijigeuza anahisi maumivu chini ya kitovu na kiuno na wakati mwingine hata kichefuchefu.

Hata hivyo,, mara nyingine tatizo hili huweza kuchangiwa na maandalizi hafifu kabla ya tendo. Endapo hakuna maandalizi yoyote basi uke unakuwa mkavu na unashindwa kufanya tendo au linafanyika kwa nguvu. 

Mbali na sababu hizo pia mwanamke huweza kupatwa na maumivu ya namna hiyo endapo mwanamke atakuwa na michubuko ukeni.

Sababu nyingine ya maumivu wakati wa tendo la ndoa kwa wanawake ni pamoja na maambukizi ukeni ambayo huweza kuambatana na kutokwa na uchafu wenye harufu na muwasho. 

Maambukizi haya huanzia ukeni na kusambaa hadi ndani ya kizazi, lakini pia yanaweza kuanzia kwa ndani hasa baada ya kuharibika au kutoa mimba. 

Hayo ni machache kuhusu tatizo hili kwa mengine mengi au ushauri unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com


No comments:

Post a Comment