Monday, 25 January 2016

BARIDI JINSI ILIVYOATHIRI MAISHA NCHINI MAREKANI

Embedded image permalink
Kumekuwepo na taarifa za watu zaidi ya ishirini kufariki kutoka na hali mbaya ya hewa iliyotokana na kuanguka kwa theluji katika miji ya Mashariki  nchini Marekani.

Hali hiyo imepelekea vituo vya dharura vya kuhudumia wagonjwa kufunguliwa kuwahudumia watu wanaopata matatizo ya mshutuko wa moyo na kuvunjika mifupa kutokana na hali hiyo.

Gavana wa jimbo la New York Adrew amewaonya madereva kutoendesha ovyo labda pale kunapokuwa na sababu za kufanya hivyo. Amesema amri ya kutosafiri iliyotangazwa hapo awali imeondolewa na viwanja vya ndege vimefunguliwa..

"Marufuku ya kusafiri imeondolewa. Hiyo haina maana watu watoke nje na kuendesha baiskeli na kuangalia hali ilivyo. Barabara zimesafishwa katika maeneo mengi. Kuna milundiko ya theluji kwenye barabara za kuingia na kutokea ambazo bado hazijasafishwa.

Mamlaka ya viwanja vya ndege imefanya kazi kubwa kusafisha viwanja vya ndege. Na sasa vipo tayari kwa ndege zitakazofanya safari.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa si Marekani pekee theluji hiyo imedondoka katika nchi nyingine za Asia kama vile Korea kusini, China ,Japan na Hong Kong.

No comments:

Post a Comment