Tuesday, 5 January 2016

FAHAMU JINSI YA KUEPUKA MATATIZO YA PUMUPumu ni miongoni mwa magonjwa sugu ya hewa yanayosumbua idadi kubwa ya watu duniani hususani watoto.

Pamoja na ukubwa wa tatizo hilo bado kuna tumaini juu ya namna ya kukabiliana na ugonjwa huo kutokana na tafiti mbalimbali ambazo zinaendelea kufanywa na wataalam wa masuala ya afya.

Kwa kawaida binadamu unapovuta pumzi, hewa huenda kwenye mdomo au pua kupitia katika mirija ya hewa na kusafiri hadi kwenye mapafu.

Katika mlolongo huu wa usafirishaji hewa kupitia mirija yake tatizo la pumu hutokea pindi njia hizo zinapoingiliwa na kitu kutoka nje na kusababisha ugumu katika upumuaji.

JINSI YA KUTIBU MATATIZO YA PUMU
a) Epuka maeneo yanayochochea shambulizi la pumu kwako kutokana na maelekezo ya daktari wako.

b) Epuka vipodozi na manukato yenye harufu kali ambayo yatasababisha pumu kwa upande wako.

c) Kula vyakula vya asili zaidi ikiwa ni pamoja na mboga  za majani kama vile nyanya, bilinganya, maharage mabichi na matango.

Kwa maelezo zaidi na ushauri unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment