Friday, 8 January 2016

GILIGILIANI HUSAIDIA KINAMAMA WENYE MATATIZO YA HEDHI


Giligiliani ni kiungo cha kawaida sana, wengi tunakitumia sana jikoni kwenye mapishi mbalimbali.

Kiungo hiki kina harufu nzuri na ladha ya uchachu kwa mbali, kiungo hiki kina vitamin A, B6, C, B12 pia inawingi wa madini ya chuma pamoja na madini ya calcium.

Kimsingi giligiliani huweza kusaidia matatizo mengi sana ikiwemo maumivu ya tumbo, pamoja na kuzuia kutapika.

Giligiliani pia inawafaa sana wanawake ambao huoata hedhi nzito, kinachotakiwa kufanyika ni kuandaa kijiko kimoja cha mbegu za giligiliani pamoja na vikombe viwili.

Changanya kwa pamoja kisha chuja halafu ongeza sukari kidogo, kisha kunywa ikiwa moto au ya uvuguvugu. Hii husaidia sana kinamama ambao wana shida ya kupata siku nzito.

Unaweza kuwasiliana zaidi na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment