Tuesday, 5 January 2016

HATIMAYE HOSPITALI YA MUHIMBILI YAPATA MASHINE MPYA YA CT SCAN


Hatimaye agizo la Rais Dkt. John Pombe  Magufuli la kupatikana kwa mashine mpya ya CT Scan katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili limeonekana kuzaa matunda baada ya Serikali kununua mashine mpya ambayo imegharimu zaidi ya bilioni 3.6 kwa pesa ya Kitanzania.

Kutokana na mashine zilizokuwepo mara ya kwanza kuharibika kila wakati Serikali imegharamia mashine mpya ambayo imeelezwa kuwa na uwezo mkubwa wa kufanya kazi tofauti na nyingine zilizowahi kutumiwa na hospitali hiyo.

Neema Mwangoko ambaye ni afisa Uhusiano wa hospitali hiyo amesema mashine hiyo mpya ina siku tatu tangu ifungwe na tayari imehudumia wagonjwa 26 mpaka sasa japo bado ipo kwenye majaribio.

Naibu waziri wa afya Dk. Hamis Kigwangala ambaye alifanya ziara katika hospitali hiyo amepongeza hatua hiyo na kutaka watendaji waboreshe huduma zinazotolewa..

No comments:

Post a Comment