Thursday, 7 January 2016

HAYA NDIO MAMBO MUHIMU YATAKAYOKUFANYA UANZE KUTUMIA VIAZI MVIRINGO KAMA TIBA

Bila shaka sote tunafahamu kuhusu viazi mviringo, au maarufu kama viazi vya 'chips' chakula kinachopendwa zaidi na mabinti wengi mjini.

Lakini je, ni wangapi tunatambua kuwa viazi hivyo mviringo vinapotumika vizuri huweza kuwa tiba ya matatizo yanatukabili katika miili yetu.

Sasa Jumamosi hii ninapenda kukupa hii faida mojawapo ya matumizi ya viazi mviringo ambavyo tumezoea kutengenezea 'chips'
Kuanzia leo kama ulikuwa hufahamu basi naomba utambue kuwa viazi mviringo ni moja ya tiba nzuri sana ya kutuliza matatizo ya miguu na nyayo kuwaka moto.

Hili tatizo la miguu kuwaka moto kati ya matatizo mengi ambayo huwasumbua watu wengi na wasijue nini cha kufanya ili kuweza kuondokana na shida hii.

Hata hivyo, hili tatizo la miguu kuwaka moto mara nyingi huwapata wale watu ambao shughuli zao huwalazimu kutembea kwa muda mrefu au kusimama kwa muda mrefu.

Miguu au nyayo kuwa na hali ya kuwaka moto huchangiwa na mzunguko dhaifu wa damu katika miguu na ukosefu wa baadhi ya virutubisho mwilini.

Sasa ili kutumia viazi mviringo, katika kutibu tatizo hili mhusika anapaswa kuosha miguu na nyayo kwa maji ya moto na sabuni na kisha kusuuza kwa maji baridi.

Baada ya hatua hiyoo andaa viazi kwa kuviponda na kupata ujiuji wake, kisha tumia ujiuji huokupaka sehemu zote ambazo unajisikia kuwaka moto.

Mara baadaya kupaka unaweza kunawa na kuosha miguu yako vizuri kwa maji safi ya baridi, lakini ikiwa utahitaji maelezo zaidi kuhusu tiba hii au tatizo hili basi wasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai sasa kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300,0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment