Saturday, 9 January 2016

HAYA NDIYO MANUFAA YA MCHAICHAI KWA AFYA YAKO


Mchaichai ni moja ya majani ambayo hutumika kama kiungo cha kuleta ladha nzuri pamoja na harufu nzuri kwenye chai.

Mchaichai umekuwa ukitumika mara kwa mara lakini ni ukweli ni kwamba wengi wetu hatufahamu umuhimu wa majani haya kiafya.

Tabibu Abdallaha Mandai kutoka Mandai Herbalist Clinic anasema kwamba matumizi ya majani ya mchaichai huwa na faida nyingi sana ndani ya miili yetu.

Tabibu Mandai ansema kuwa mchaichai husaidia sana kurekebisha mfumo wa umeng'enyaji wa chakula ndani ya mwili.

Aidha, mchaichai pia husaidia kuondoa kiungulia na kuzuia kutapika kwa wale wanopatwa na kichefuchefu mara kwa mara.

Pia matumizi ya chai ya mchaichai husaidia sana kuondosha sumu za mwilini na hivyo kulinda zaidi afya ya figo.

Sambamba  na hayo kutumia majani ya mchaichai pia husaidia sana kuondosha maumivu ya mwili katika sehemu mbalimbali.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment