Friday, 15 January 2016

HUU NDIO UWEZO WA MAUA YA MLONGE KATIKA MATIBABU

Mlonge ni mti ambao una asili ya India, lakini kwa sasa mti huu hupandwa kanda za tropiki. 

Karibu kila sehemu ya mti huu ni tiba yaani kuanzia mbegu zake, magome, majani, maua pamoja na mizizi. Sasa leo hapa mimi nitazungumzia kuhusu maua tuu!!
 
Maua ya mti wa mlonge nayo yana msaada wake katika matibabu na miongoni mwa faida kubwa ya maua haya ni kumsaidia mama anayenyonyesha kuongeza kiwango cha utokaji wa maziwa.

Sambamba na hayo, maua ya mlonge pia husaidia kutibu matatizo ya haja ndogo (mkojo) kutoka kwa shida au ikiambatana na maumivu, kwahiyo matumizi ya maua huweza kuondosha tatizo hilo.

Maandalizi ya maua haya ya mlonge katika tiba inabidi yachemshwe na kupata mfano wa chai iliyotokana na maua ya mlonge ambayo mhusika atahitajika kunywa chai hiyo kila siku kikombe kimoja asubuhi na jioni.

Hayo ndiyo machache ambayo nimeona nikwambie leo mdau wangu, lakini kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmanditz@gmail.com

No comments:

Post a Comment