Monday, 18 January 2016

JE, UNAFAHAMU FAIDA ZA MAJANI YA MPERA NA PERA LENYEWE KATIKA MATIBABU? MAJIBU YAPO HAPA


Mapera ni moja ya tunda maarufu sana na linafahamika na watu wengi. Tunda hili asili yake ni katika nchi ya Asia, lakini pia hupatikana katika nchi za Magharibi.

Mapera ni miongoni mwa matunda yenye kiwango kizuri cha vitamin C pamoja na vitamin A na inaelezwa kuwa kiwango cha vitamin C kinachopatikana  ndani ya mapera ni sawa na mara nne ya kiwango cha vitamin hiyo inayopatikana kwenye chungwa.

Pia mapera yamesheheni virutubisho mbalimbali ikiwa ni pamoja na vitamin B2, E na K pamoja na madini ya chuma, copper, potassium na manganese.

Kwa mujibu wa utafiti uliowahi kuchapishwa na jarida la Journal of Human Hypertension mwaka 1993 ulieleza kuwa tunda aina ya pera huweza kupunguza kiwango cha msukumu mkubwa wa damu ndani ya mwili yaani High Blood Pressure hii ni kwa sababu ya madini ya potassium na vitamin C ambayo husaidia kuweka sawa msukumo wa damu ndani ya mwili.

Pia majani ya mpera yanapoandaliwa kama chai yaani yakichemshwa husaidia sana kuondosha sumu ndani ya mwili 'cholesterol' jambo ambalo husaidia sana kulinda afya ya moyo wako.

Majani hayo hayo ya mpera pia husaidia sana wale wenye tatizo la kuharisha hii ni kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2008 uliochapishwa kwenye jarida the Revista do Instituto de Medicina Tropical de São Paulo, ambao walieleza kwamba majani hayo ya mpera yanauwezo wa kuzuia vimelea vya staphylococcus aureus ambavyo huchangia tatizo la kuhara.

Hivo basi mgonjwa wa kuhara huweza kuandaliwa maji yatokanayo na majani ya mpera ambayo yamechemshwa na kunywa kikombe kimoja asubuhi na jioni.

Hayo ndio machache kuhusu mpera kwa mengine mengi unaweza kuwasiliana na Tabibu Abdallaha Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment