Saturday, 30 January 2016

JINSI YA KUJITUNZA WAKATI WA UJAUZITO AU KUNYONYESHA

Habari za Jumamosi hii mpendwa msomaji wetu wa www.dkmandai.com napenda kukupa pole kwa kazi za wiki nzima, huku nikiamini kuwa baadhi yenu leo mpo katika mapumziko, lakini kama upo kazini pia si mbaya.

Mara nyingi siku za weekend huwa napenda kuzungumzia vitu vya kawaida kabisa vinavyotuzunguka katika maisha yetu ya kila siku na leo nimeona nianze na hili la wanawake wajawazito au wale waliojifungua.

Wanawake wengi wanapokuwa wakati wa kipindi cha ujauzito hujikuta wakianza kutojijali na kijiweka hovyo hovyo jambo ambo huchangia wengi wao kupoteza mvuto.

Baadhi yao hujikuta wakiendelea kuwa katika hali hiyo hata mara baada ya kujifungua na ukimuuliza kwanini atakwambia analea.

Kimsingi ni kwamba kujifungua au hali ya kuwa na ujauzito haifai kuwa sababu ya mwanamke kupoteza mvuto aliokuwanao hapo awali. Hivyo ni vizuri mwanamke unapokuwa katika hali hiyo ukahakikisha unabaki katika muonekano wako ule ule wa awali.

Kumbuka kuwa katika kipindi hiki cha ujauzito au kulea unaweza kutumia vipodozi visivyo na kemikali na ukaendelea kuonekana vizuri tu.

Pia ni vizuri kutumia muda mwingi kufanya mazoezi mepesi mepesi ambayo husaidia sana kukuweka katika ‘shape’ nzuri pamoja na hali ya ujauzito ulio nao kazi ya kulea.

Zingatia kwamba wakati wa ujauzito mama hupaswi kupaka vipodozi vyenye kemikali, kwani huweza kusababisha madhara kwa mtoto.

Mama aliyejifungua naye anapaswa kuepuka kupaka mafuta, yenye harufu kali inayoweza kuwa na madhara kwa mtoto na wakati wengine kumsababishia mtoto wakati mgumu katika kupumua.

Ndugu yangu kama unateseka na magonjwa mbalimbali ni vyema ufanye utaratibu wa kuwahi kufika Mandai Herbalist Clinic sasa ili upate suluhisho la matatizo yako ya kiafya. Wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongo la ndege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment