Thursday, 28 January 2016

KWA WALE WENYE KICHEFUCHEFU UNAWEZA KUTUMIA KARAFUU PIA

Karafuu ni kiungo ambacho hupatikana sana hapa nchini hususani Zanzibar, huku kiungo hiki kikiweza kutumika peke yake au kwa kuchanganywa na viungo vingine.

Kiungo hiki kina sifa ya kuwa na ‘carbohydrates’ protini, mafuta (Volatile oil), nyuzi nyuzi ‘fiber’ ‘calcium,’ madini chuma na ‘potassium,’ pamoja na vitamin vitamin A na C.

Karafuu pia husaidia kuboresha uyeyushwaji wa chakula tumboni, huku ikisaidia pia kupunguza kichefuchefu, kutapika na kuharisha.

Sambamba na hayo, karafuu husaidia kulinda kuoza kwa meno na kufanya kinywa kuwa na harafu nzuri.

Unaweza kutumia kiungo hiki katika juisi ya matunda yenye uvuguvugu, supu, mchuzi au vinywaji vingine vilivyochemshwa.

Tafadhali endelea kuwa karibu nasi kwa kulike ukurasa wetu wa facebook uitwao Mandai Herbalist Clinic- mhc, ambapo utakuwa ukifikiwa na taarifa mbalimbali za tiba hususani tiba asilia, lakini pia kama unasumbuliwa na magonjwa sugu wasiliana na Dk Mandai kwa simu namba 0652 163 838, 0716 300 200, 0783 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment