Monday, 18 January 2016

MADHARA YANAYOWEZA KUTOKEA KUTOKANA NA MATUMIZI MABAYA YA SIMU


Ulimwengu wa sasa mawasiliano ya simu ni jambo la msingi sana na karibu kila mtu hivi sasa kwa namna moja au nyingine hujikuta akilazimika kutumia simu katika maisha yake.

Hata hivyo, pamoja na umuhimu wa mawasilianao hayo, lakini kumekuwepo na tafiti ambazo zinaeleza kuwa matumizi ya simu sana huweza kuwa na madhara kiafya kutokana na mionzi inayopatikana kwenye kifaa hicho.

Kutokana na mawasiliano haya kuweza kuchangia madhara mbalimbali kiafya kuna baadhi ya hizi njia ambazo hupendekezwa kuzingatia wakati wa matumizi ya simu.

Pendelea kutuma ujumbe mfupi wa maneno (sms) zaidi ya kupiga simu, licha ya kwamba watanzania wengi si wapenzi sana wakuandika sms lakini inashauriwa zaidi kutumia sms kuliko kupiga simu.

Ukiweza kuepuka kupiga simu zaidi basi utakuwa umelinda hata afya ya masikio yako na badala yake ukaamua kuwasiliana na mtu kwa kutumia sms.

Usilale karibu na simu wakati wa usiku kwani kuna mionzi hatari ambayo huzunguka muda huo, lakini pia epuka ni nzuri kama una mazungumzo ya muda mrefu basi ni njema ukatumia earphone.No comments:

Post a Comment